Tupokigwe
Abnery Mwampondele amezaliwa,Seronera - Serengeti mkoani Mara.Alisomea
shahada ya Isimu ya lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwa
sasa ni mwalimu wa somo la Kiswahili katika shule ya Sekondari ya
Wasichana Precious blood iliyopo mkoani Arusha-Tanzania. N’je na kazi ya
uwalimu Tupokigwe Abnery ni mtunzi wa vitabu vya hadithi, mbunifu wa
mavazi ya kiasili, mjasiriamali na mwandishi wa gazeti tando (blogger)
inayoitwa Sinyati Blog.
Tupokigwe
Abnery alikuwa na kawaida ya kupenda kujibembeleza au kujifariji akiwa
anatembea kwa kutengeneza hadithi katika fikra zake ili kuweza kulala au
kufika anakoelekea bila kuchoka,ndipo siku moja baada ya kushiriki
shindano la uandishi wa Riwaya fupi kwa wanafunzi wa shule ya
msingi,sekondari na vyuo vikuu Tanzania kwa ajili ya Tuzo ya mama Salma
Kikwete iliyoandaliwa na TASAKI(Tamasha la Sauti ya Kiswahili) aliibuka
mshindi wa pili wa riwaya fupi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.
Hivyo
hiki kitabu ni muendelezo wa Riwaya aliyopatia Tuzo.Soma kitabu hiki
uweze kujionea ubunifu wa hali ya juu wa fani pamoja na mshikamano wa
maudhui uliyopo ndani ya kitabu hiki.
Mapenzi
Kaburini ni kitabu chenye mtazamo yakinifu,ni kitabu ambacho maudhui
yake yamezitazama nchi za Afrika Mashariki na changamoto zilizopo katika
nchi kwa upande wa viongozi pamoja na wananchi.Kimebeba maudhui
yanayowalenga wananchi wote bila kujali utabaka.Kwa upande wa fani
kimetumia majina ya halisi na kubuni hasa kwa upande wa maeneo ya miji
mfano kuna miji kama Kinyonga,kupe,chatu ambayo ni majina yaliyopo
katika nchi ya Simba.Nchi hii ya Simba ni nchi inayosimamia nchi
zilizopo Afrika Mashariki.
Mbali
na hilo pia visa na matukio vimepewa majina ya hifadhi za Taifa
zilizopo katika nchi ya Tanzania.Mfano hifadhi ya Ruaha,Sanane,Manyara
na kitulo kama ukisoma kitabu hiki utagundua kuwa sifa ya hifadhi
inaendana na visa na matukio yaliyopo katika sehemu hiyo iliyoandikwa
kwa jina la hifadhi.Mfano hifadhi ya Kitulo inasifika kwa kuwa na
maua,kama tujuavyo maua huashiria sifa nyingi moja wapo hapo ni
upendo,watu wengi hutumia maua katika kuwapa wapenzi wao,mfano kuomba
msamaha,kumfariji mtu,hata kuonesha upendo kwa mtu unayempenda.
Utakaposoma
kitabu hiki utaburudika na kufundishwa baadhi ya mambo kama Kukuza
imani yako kwa Mungu,uaminifu katika ndoa,uzalendo katika nchi yako na
Madhara ya kujihusisha katika mahusiano na mtu usiye mjua.
Nitakupatia kionjo kidogo katika sura ya kwanza ili kuweza kuona mwanzo tu wa hadithi hii ambayo hutapenda kuacha kuifuatilia:
Sura ya kwanza
Hifadhi ya Sanane
Ilikuwa
siku ya Jumatatu katika ghorofa la tajiri mmoja, mmiliki wa hoteli
maarufu katika nchi ya Simba. Tajiri huyo alifahamika sana kwa kuwa
alikuwa akijitolea sana kwa wananchi wasiojiweza, katika miji mbalimbali
ya nchi hiyo.Watu husemamfadhili punda kuliko mwanadamu vilevile tenda
wema kisha nenda zako baraka utazipata kwa Mungu,usisubiri hisani za
wanadamu.
Pamoja
na misaada aliyoitoa kwa watu mbalimbali lakini wananchi wa Simba
hawakujali misaada yake, walimteta kila kona kuwa anatumia nguvu za giza
na amekwisha toa kafara ndugu, jamaa na hata watoto wake ili kujipatia
utajiri mkubwa alionao. Siku hiyo ya Jumatatu katika pagala la tajiri
huyo aliyefamika kwa jina la Pesa nyingi.
katika
moja ya chumba cha ghorofa hilo kulikuwa na mwanamke mrembo na mzuri
sana wa sura, mrefu mithili ya twiga, mwenye umbo zuri la kiafrika,
chini alikuwa amevaa suruali ya chupa huku akiwa amevaa blauzi tatu juu
zenye rangi tofauti na nywele timutimu zikiwa zime nakishiwa na vitu vya
jaani kama vichana,visude, rasta chakavu na kufungwa kitambaa cha
kitenge aina ya makenzi ,uso wake ulikuwa kama paka mwenye madoa
kutokana na kujipamba kwa majivu na masizi ya mkaa wa jaani. Pembeni ya
ua hilo alikuwepo mnyama mwenye maringo
mbugani
kuliko wote, sio mwingine bali ni kijana mtanashati aliyekwenda
hewaani, rangi ya ngozi yake nyeusi ya kung’aa. Tabasamu la mwanaume
huyo lililokuwa likimfariji mtoto mzuri, lili mvutia sana Savannah.
Ghafla ilisikika sauti ya mwanamke huyo ikiita kwa sauti ya chini
iliyojaaa simanzi na mateso ya muda mrefu,ilisema “John naumia mume
wangu, hali yangu kila kukicha afadhali ya jana”.
John
alijibu “usijali Savannah nipo hapa mke wangu kwa ajili yako utapona tu
tutakwenda hospitali,subiri nikuandalie chakula ule, kisha nikupeleke
hospitali malikia wangu”. Basi baada ya John kumfariji Savannah aliamka
na kuelekea jikoni pembeni ya sehemu aliyokuwa amelala mpenzi wake.
Watu
hawa walipendana sana ni vile tu hali yao haikuwa nzuri kifedha
waliishi kwa kuhangaika, kuomba msaada na wakati mwingine walifukuzwa na
walimwengu pale walipokuwa wakiomba msaada, watu waliwapita kama mbwa
waliokosa matunzo.
Wapenzi
hao Walizoea maisha ya kuokota vyakula jalalani na kukimbilia magari ya
taka sambamba na kusubiria mabaki ya chakula katika migahawa
mbalimbali. Wakati huo John alikuwa akitimiza ahadi aliyo mhahidi
malikia wake alimuandalia chakula walicho kiokota katika soko kuu la mji
huo wa Chatu. John alimuinua Savannah pale alipokuwa amelala kwenye
kanga chakavu akiwa amejifunika magunia yalionekana ni ya mpunga. John
alimlisha Savannah chakula kile ambacho hawakujua kilipikwa lini na
kutupwa na nani na lini. Savannah alisikika akisema “asante mume wangu
hata
mwanangu
anafurahi sasa naona napata nafuu, nahisi ni njaa ilikuwa inaniuma”.
Mwanangu nisamehe mama kakushindisha njaa, nakupenda sana najua wewe
utakuwa mrembo zaidi yangu mwanangu hata baba yako anakupenda”. John
alikuwa anapenda sana utani alicheka na kusema “atakuwa mrembo kama wewe
kweli mke wangu lakini rangi ya ngozi yake itakuwa kama yangu, yako iko
kama ya nguruwe hahahaaaa!” Savannah alikuwa mweupe kama Nguruwe,
ingawa alivyokuwa anaonekana ni kama mtu mwenye ngozi ya rangi ya maji
ya kunde kutokana na ugumu wa maisha.
Wawili
hao walifurahi pamoja na kusahau shida walizokuwa nazo.Walipomaliza
kula wapenzi hao waliamua kutoka nje baada ya kukaa ndani ya paghala
hilo kwa muda wa wiki moja, Dikidiki hao walikuwa na kaida ya kufanya
hivyo wanapotafuta riziki na kujilimbikizia ndani ya paghala lao kisha
wana kaa kwa muda huo bila kutoka. Usilolijua ni kama usiku wa kiza,
basi Savannah na John walipotoka wakiwa n’je ya mgahawa mmoja uliokuwa
unapendwa sana na wananchi wa mji huo wa Chatu zilisikika sauti za
wanawake wakisema:
“haya
jamani sasa ni ule wakati wa Pesa nyingi kuingiza hela sasa wenzi
wametoka fungate”. Waliamini kuwa Pesa nyingi alikuwa anawatumia
Dikidiki hao kama misukule inayotoka na kurudi ndani na wanapotoka basi
mzee Pesa nyingi huingiza hela nyingi sana. Kwakuwa wenzi hao walikuwa
hawaelewi kinachoongelewa waliendelea kuomba msaada kwa wateja
waliokuwepo hapo mgahawani. Wanapokosa waliamua kucheza baadhi ya nyimbo
zilizokuwa
zikipigwa
katika mgahawa huo, wakicheza hupewa chakula na fedha ambazo hutoka
katika mifuko ya wateja. John alikuwa anapenda sana kucheza,wakiwa
wamekaa chini walisikia wimbo wa mwanamuziki maarufu Tanzania Diamond
unaosema Je, Utanipendaga? John alimuinua Savannah aliyeonekana kachoka
na mimba yake. Savannah aliamka na kucheza na mpenzi wake ,walicheza kwa
miondoko ya kihindi, machozi yalisafisha uso wa Savannah huku yakiosha
kifua cha John kilichokuwa kimejaa kama mlima na mikono iliyokuwa na
miinuko ya kupanda na kushuka ilizunguka juu ya kifua cha Savannah na
kumfanya ahisi kazungukwa na jeshi kubwa la malaika wa ulinzi.
Baada
ya kumaliza kucheza savannah alikuwa amechoka sana, kitendo cha kucheza
kilimsababishia kuchokoza maumivu na kupelekea kupata uchungu katika
kizazi chake. Baada ya kuona hivyo John aliinama na kuchukua zawadi
walizozipata kutoka kwa hadhira iliyokuwa ikiwatazama huku baadhi ya
hadhira wakibubujikwa na machozi walimpelekea hela na chakula John
katika kapu lake la kukusanyia riziki. Watu waliokuwa wakiwatazama
Savannah na John hawakujali maumivu ya mwanamke yule na kuona kawaida.
Wapo
waliosikika wakisema hawa vichaa wana akili, wengine walisema hawa si
vichaa, vichaa gani wana akili ya kutafuta hela hivi, wamekusanya umati
mkubwa hivi na kuwafanya watu kutoa kile walichonacho. Mama mmoja mwenye
busara anayeuza katika mgahawa huo aliyefahamika kwa jina la mama ndaga
akasema“Jamani mimi nawafahamu hawa vichaa kwanza hawakuwa wakitembea
hivi pamoja kama Dikidiki, huyo kaka unayemuona alikuwa..........pata
mwendelezo kwa kujipatia kitabu hiki.
Nicheki kwa mawasiliano haya:+255756377940
Instagram: @sinyatiblog
Facebook:Tupokigwe Abnery
0 Comments