Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira,
Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha
kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited leo Machi 7, 2018,
wakati wa ziara yake ya kushtukiza kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi
ipasavyo Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, ikiwa ni pamoja na wale
ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
NA K-VIS BLOG/KHALFAN
SAID
SERIKALI
imesitisha shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda cha kutengeneza mifuko ya
nailoni (viroba), cha TASIPA kilichoko jijini Dar es Salaam kwa siku 14 kuanzia
leo Machi 7, 2018 baada ya kubainika kuwa kiwanda hicho kinahatarisha maisha ya
wafanyakazi wake.
Sambamba
na hilo, kiwanda hicho pia kimetozwa faini ya shilingi milioni 18 kwa kukiuka sheria
ya usalama na afya mahala pa kazi.
Aidha
Mhe. Mavunde pia amevitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 22.8 viwanda vya
Hengji Investment, ambacho pia kinatengeenza viroba (mifuko ya nailoni), na
kiwanda kingine cha kutengeneneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited kwa
makosa mbalimbali ya kukiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini.
“Katika
kukagua Sheria za usalama na afya mahala pa kazi, tumebaini kuwa mazingira ya
kiwanda hiki cha TASIPA ni hatarishi mno kwa mfanyakazi kufanya kazi na tayari
watu wa OSHA walikwishafika hapa na kutoa maelekezo, lakini hakuna
kilichofanyika.” Alisema Mhe. Mavunde.
Naibu
Waziri pia aliagiza kuwa muajiri huyo kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi
wote kwa mujibu wa sheria namba 6 ya mwaka 2004 na mikataba iwe imekamilika n
dani ya siku 14 na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi ili aipitie.
Awali
Mheshimiwa Mavunde alitembelea kiwanda
cha kutrengeenza nywele na kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa
wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mikataba ya kazi, kufanya kazi kwa
muda mrefu bila kulipwa malipo ya muda wa ziada na kufanya kazi kwenye
mazingira ambayo yanahatarisha afya za wafanyakazi.
Kiwanda
hicho kilitozwa faini ya shilingi milioni 8 na kutakiwa kurekebisha kasoro zote
zilkizojitokeza ndani ya kipindi kifupi.
Naibu
Waziri pia alikitoza faini kiwanda cha Hengji Investment Limited
kinachojishughulisha na utengenezaji mifuko ya viroba kwa ukiukwaji mkubwa wa
sheria za kazi na usalama mahala pa kazi.
Ziara
ya Naibu Waziri ambayo imeianza wiki iliyopita jijini Mwanza, inalenga
kufuatilia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziriu Mkuu, anayeshughulikia
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama
aliyoyatoa Mwishoni mwa mwaka jana, kuwataka waajiri wote ambao hawajajisajili
na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), watekeleze wajibu huo wa kisheria
vinginevyo wafikishwe mahakamani.
Tayari
waajiri kadhaa wameanza kufikishwa mahakamani kwa kosa hilo na operesheni hiyo
kwa mujibu wa Naibu Waziri ni endelevu na itafanyika nchi nzima.
Kwa
mujibu wa sharia ya usalama mahala pa kazi mfanyakazi huyu alipaswa
kuvaa mask na gloves. hapa ni kiwanda cha TASUPA kinachotengeneza mifuko
ya nailoni (viroba)
Naibu Waziri Mvunde akishuhudia ukiukwaji wa sharia ya usalama mahala pa kazi kiwanda cha TASUPA
Naibu
Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa
Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo,
akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya
kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda
cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).
Naibu
Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa
Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo,
akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya
kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda
cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).
Wafanyakazi
wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH Afrique Tanzania Limited,
wakimsikiliza Naibu Waziri Mabunde(hayupo pichani) alipozunhgumza nao.
Naibu Waziri Mvunde, alipotembelea kiwanda cha SH Afrique
Kamishna
wa Kazi, Bi.Hilda Kabisa, (kushoto) akizunhguzma jambo.Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bi.
Rehema Kabongo.
Msaidizi
wa Meneja Mwajiri kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique
Tanzania Limited, Bi.Domina Domisium, (kulia), akitoa maelezo ya
uendeshaji wa kiwanda hicho, mbele ya Naibu Waziri Mhe. Mavunde
Bi. Kabisa akimuhoji Bi.Domina
Naibu
Waziri Mvunde, akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji kiwanda cha SH.
Afrique Tanzania Limited, Bi.Kim Minju, (kulia). Katikati ni Bi. Rehema
Kabongo.
Mhe. Mavunde akizungumza na wafanyakazi wa SH. Afrique Tanzania Limited.
Wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba) cha TASUPA.
Naibu Waziri akitoa maagizo kiwanda cha TASUPA.
Mmoja
wa wafanyakazi wa kiwanda cha TASUPA, kwa niaba ya wenzake akizungumza
mbele ya Naibu Waziri, ambapo alieleza ukiukwaji mkubwa wa haki za
wafanyakazi kiwandani hapo.
0 Comments