IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana.
DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.
DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange
Dar es Salaam, Februari 24, 2015
MWANAMKE mchuuzi wa mboga mboga katika Soko jipya la Kawe jijini Dar
es Salaam, Grace Pascal Kalengera, jana alikuwa miongoni mwa wakazi
watatu wa Dar es Salaam waliokabidhiwa zawadi zao baada ya kushinda
promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi.
Ijumaa iliyopita, Grace alipigiwa simu na Balozi wa Airtel Yatosha
Zaidi, mwigizaji maarufu nchini, Lulu, baada ya namba yake kuwa
miongoni mwa washindi kwenye droo iliyochezeshwa makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kuigiza nchini.
Siku nne tu baadaye, leo Jumanne, Meneja Masoko wa Airtel, Frederick
Mwakitwange, alimkabidhi gari lake mama huyo aliyeonekana wazi akiwa
na furaha isiyo kifani.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwakitwange alisema: “Sisi Airtel,
tunafarijika sana tunapowaona washindi wakimiminika ofisini kwetu kila
wiki kujichukulia zawadi zao. Na kwa ukweli zawadi ya gari si zawadi
ndogo kwa wengi miongoni mwetu.
“Tuliamua kwa makusudi kabisa kutoa magari kama zawadi kwa washindi
kwa lengo la kuonyesha nia yetu ya kuboresha na kuyabadili maisha ya
Watanzania.” Mbali na Grace, washindi wengine waliokabidhiwa magari yao ni pamoja na John Freddy Kiwale mkazi wa Kinondoni ambaye pia ni wakala wa Airtel Money na Donald Fred Baruti mfanyabiashara wa Mwembechai
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, alitoa wito kwa wateja wa
kampuni hiyo kuendelea kutumia huduma za Airtel Yatosha Zaidi waweze
kupata nafasi ya kujishindia magari.
“Kama mnavyoona, hata mawakala wa Airtel Money wanaweza kushinda. Hii ni kwa sababu tu kwamba nao pia ni wateja wetu. Inafahamika kuwa kuna vigezo na masharti katika kushiriki na sisi tunazingatia sana hilo,”
alisema Mmbando.
Washindi wengine wa wiki iliyopita watakaopewa magari ya oleo ni Simon
Grayson (Yombo, Kisiwani), Bilal Juma Mlendela (Tabata) na Maxbeth
Isack Manene (Tabata Segerea), kisha mkazi na mkulima kutoka Bukoba,
Kajala Kokutima Said, naye atapewa gari wiki hii.
Tayari magari 17 kati ya 60 yamekwishapata wamiliki wake wapya.
0 Comments