Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa
huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo
zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya M-Pesa na Tigo kupitia
huduma yake ya Tigopesa. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo
Tanzania, Diego Gutierrez.
Meneja
Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia) akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano
ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya
malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya Tigopesa na
Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa. Anaeshuhudia kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto, aliyekaa) na Meneja
Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia, aliyekaa), wakitia saini
mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na
miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia
huduma ya M-Pesa na Tigopesa. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo
cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa
Chapa ya Tigo, William Mpinga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili toka kushoto) na
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, wakibadilishana nakala za
mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na
miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia
huduma ya M-Pesa na Tigopesa, wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo
cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa
Chapa ya Tigo, William Mpinga.
Huduma
za kutuma na kupokea fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo
zinazotolewa na makampuni ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya
M-Pesa na Tigo kupitia huduma yake ya Tigopesa zitazidi kuimarika
kutokana na makampuni hayo kuingia makubaliano ya kutoa huduma hizo kwa
ushirikiano.Ushirikiano huo utawawezesha wateja wa makampuni hayo
kutuma na kupokea fedha na kufanya mihamala ya malipo moja kwa moja.
Makubaliano
hayo ambayo yametangazwa leo yatawawezesha mamilioni ya wateja
wanaotumia huduma za M-Pesa na Tigopesa kupata huduma kwa ubora zaidi
kwa kuwa mteja akipokea au kutaka kutuma pesa au kufanya malipo
hatolazimika kutoa fedha kwenye mtandao mmoja kwenda mwingine kama
ilivyo sasa bali atafanya akitakacho moja kwa moja na bila kutozwa
malipo ya ziada.
Akiongea
leo wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania, Rene Meza alisema “Haya ni mapinduzi makubwa katika
kutoa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi nchini Tanzania.
Katika siku za karibuni wateja wa makampuni haya mawili wataweza kutuma
na kupokea fedha na kufanya mihamala ya malipo mbalimbali moja kwa moja
bila kulazimika kuzitoa kwa mawakala kwanza na kuziingiza kwenye huduma
ya fedha ya mitandao yao kama ilivyo sasa.”
Wateja
wa M-Pesa hivi sasa wanaweza kulipia huduma mbalimbali baadhi yake
zikiwa ni kulipia ving’amuzi vya televisheni zao, nauli za usafiri wa
ndege, huduma za bima, huduma za maji na umeme, kodi mbalimbali za
serikali, karo za shule, kurejesha mikopo katika mabenki na uchangiaji
katika mifuko ya pensheni.
“Huduma
hizi hivi sasa zinatumiwa na watu wengi na kwa kipindi cha miaka saba
tangu zianzishwe zimeleta mapinduzi na kurahisisha maisha ya Watanzania
kwa kiasi kikubwa. Tuna imani kwa kushirikiana na Tigo katika huduma hii
tutanufaisha wateja wa makampuni haya mawili kwa kiasi kikubwa na hivi
sasa tuko katika mchakato wa kuboresha mfumo wetu wa M-Pesa ili ifikapo
mwisho wa mwaka tutakapoanza kutoa huduma hizi pamoja kusiwepo na
matatizo yoyote ya kimtandao na tutawekeza kiasi cha shilingi Bilioni
150/-kwa kazi hii,” alisema
Meza
aliongeza kuwa kushirikiana kwa makampuni haya mawili katika kutoa
huduma za pesa hakutaongeza gharama kwa watumiaji wa Tigopesa na M-Pesa
bali kutawarahisishia kupata huduma bora na kwa karibu kutokana na
mtandao mkubwa wa makampuni haya mawili yanayotoa huduma za mawasiliano
nchini.
“Tunachofanya
hivi sasa ni makampuni haya kujipanga kuhakikisha yatakapoanza kutoa
huduma za kifedha kwa pamoja mwishoni mwa mwaka huu yanatoa huduma za
uhakika. Mtandao wetu wa mawakala 85,000 wa M-Pesa kwa sasa unahudumia
zaidi ya wateja milioni 7 ambao wanafanya shughuli mbalimbali
zinazochangia kukua kwa uchumi wa Taifa na tumejipanga kuhudumia wateja
wengi zaidi kwenye miaka ya mbele,” alisema Meza.
Kwa
upande wake Meneja Mkuu wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo,Diego
Gutierrez alisema ushirikiano huu utawanufaisha wateja wengi wa
makampuni haya mawili na kuwarahishia maisha na kuwawezesha kufanya
biashara zao vizuri wakati huo huo fedha zao zikiwa salama
“Tuna
imani kwa kushirikiana na Vodacom katika huduma hii tutanufaisha wateja
wa makampuni haya mawili kwa kiasi kikubwa na tutahakikisha wateja wetu
wanaendelea kupata huduma bora za kifedha kwa njia ya mtandao bila
kuingia gharama ya ziada na tuna uzoefu wakufanya kazi katika
ushirikiano kama huu kwa kuwa tayari tunashirrikiana na makapuni ya
Airtel na Zantel na wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma
nzuru.Tunashukuru Benki Kuu ya Tanzania na Taasisi ya IFC kwa
kufanikisha utaratibu huu wa makampuni haya kutoa huduma kwa pamoja
”.Alisema Gutierrez
Huduma
za M-Pesa na Tigo Pesa kwa sasa zinatumika kulipia huduma mbalimbali
baadhi yake zikiwa ni kulipia ving’amuzi vya televisheni zao, nauli za
usafiri wa ndege, huduma za bima, huduma za maji na umeme, kodi
mbalimbali za serikali, karo za shule, kurejesha mikopo katika mabenki
na uchangiaji katika mifuko ya pensheni.
Shirika
la Kimataifa la Fedha (IFC) limekuwa likiunga mkono kuimarishwa kwa
huduma hizi za fedha kwa njia ya simu na hicho ndicho chanzo cha
makampuni haya kuingia makubaliano ya kuunganishwa kwa huduma hizi
nchini Tanzania ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
0 Comments