TPB yaunganisha matawi yake na Mkongo wa Taifa


Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia). Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia). Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa.Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini.Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya TPB Dar es Salaam. Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya TPB Dar es Salaam.Baadhi ya Maofisa wa TTCL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini. Baadhi ya Maofisa wa TTCL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) pamoja na Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge wakipongezana kwenye hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) pamoja na Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge wakipongezana kwenye hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.Picha ya pamoja ya maofisa wa TPB na TTCL walioshiriki katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini. Picha ya pamoja ya maofisa wa TPB na TTCL walioshiriki katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.

  Na Mwandishi Wetu 

  BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imedhamiria kuunganisha matawi yake yote katika mfumo wa kisasa wa mawasiliano kupitia mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) ili kuberesha huduma na mawasiliano katika huduma zake. 

 Taarifa hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa alipokuwa akizungumza katika makabidhiano ya mradi mpya wa benki hiyo uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. 

 Tawa alisema mpaka sasa matawi ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo na Kijitonyama tayari yameunganishwa kwenye mfumo huo mpya na wa kisasa kimawasiliano.

 "..Mpaka hivi sasa matawi yetu Kumi na Moja (11), yakiwemo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo, Kijitonyama, tayari zimeunganishwa kwenye mfumo huo.

 Hii ni katika hatua ya mwanzo tu ya mradi huu, kwani benki ya Posta imekusudia kuyaunganisa mtawi yake yote kwenye mfumo huu," alisema Tawa. Alisema baada ya kukamilisha matawi ya TPB katika mfumo wa Mkongo (Fiber Optic), imepata mafanikio makubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo matawi haya yalikuwa yameunganishwa na mtandao wa teknolojia ya Copper (Copper network). 

 Aidha akizitaja faida ambazo benki hiyo imezipata baada ya kujiunga na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unaosimamiwa na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni pamoja kupungua kwa msongamano wa wateja kusubiria huduma kwenye matawi, kuongezeka kwa ufanisi na kupungua kwa dharura ya kusitisha huduma kwa muda. 

 "...Pia tumeboresha uwezekano wa kutambua tatizo lolote linalotokana na kukatika kwa mawasiliano kwani huu ni mfumo wa kidijitali...kupungua kwa gharama za uendeshaji katika benki yetu." alisema Tawa. 

 Kwa upande wao TTCL ikikabidhi mradi huo kwa TPB, Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard alisema mfumo huo wa mkongo unafaida kubwa kwani, mbali na kuwa salama zaidi pia unauwezo wa kugundua tatizo la mawasiliano kabla ya kutokea hivyo kufanyiwa kazi mapema. 

 Alisema hata hivyo alisema njia za kupitisha mawasiliano hufanya kazi kwa kutegemeana na zipo zaidi ya moja hali ambayo huwezesha hata njia moja kuisaidia nyingine inapopata tatizo huku tatizo lililojitokeza likishughulikiwa kwa wakati huo. 

 Faida hizo pamoja na nyingine nyingi zinaifanya benki ya Posta iamini kuwa huduma hii ya Mkongo itolewayo na TTCL ni bora nchini na itatusaidia sana sisi benki ya Posta kuboresha huduma zetu na kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za kibenki.

Post a Comment

0 Comments