Hapa
ilikuwa ni mapema kabisa ambapo washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa
Chakula msimu wa Nne wakiwa wanajikusanya kwa ajili ya kupewa mwongozo
wa siku nzima
Baada
ya washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano linalo
endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na kudhaminiwa na Gates
and Melinda Foundation,TBS, Cooperative Bank Great Britain na Care
Tanzania, baada ya kuwasili wote sasa wanapangwa makundi makundi kwa
ajili ya kuanza mchakato wa siku
Hapa
katika kundi la kwanza washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
, Shindano linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow hapa
wakiwahamasisha wanakijiji cha kisanga kilimo cha Biashara na
kubadilishana mawazo kuhusu nyenzo , mazao na tathimini ya mapato na
matumizi.
Kundi la pili wakiendelea kutoa Elimu ya Kilimo kwa Wanakijiji
Kundi la tatu wakiendelea kutoa elimu na kubadilishana mawazo na wanakijiji wa kijiji cha Kisanga
Mmoja
wa Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula , Regina
kalipi(Katavi) akiwa ameshikiriwa na washiriki wenzake baada ya
kuanguka akisoma Lisara iliyokuwa inahusu kilimo
Katikati ni Winnie Malya Mshiriki kutoka Kilimanjaro akisoma Lisara kwa wanakijiji ambao hawapo Pichani juu ya kilimo.
Burudani
lilianzia hapa ambapo Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Pili Kashinje(zanzibar, Neema Hilonga (Manyara) na Mandutha kitoeloh
9Singida) walishiundana vilivyo katika kukimbia lakini Pili aliibuka
kuwa Mshindi.
Burudani
ilizidi kuwa Taaamu zaidi ambapa Washiriki wa shindano la Mama Shujaa
wa Chakula Shindano linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya
Grow na kurushwa katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa
12:30 Jioni na Kurudiwa saa 11:30 asubuhi , hapa ni pata ni kupate
ambapo Winnie Mallya(Kilimanjaro) Edna Kiogwe (Dar es salaam) na
Severina Mutahyabarwa (Kagera) walishindana vikali kukukimbia wakiwa
wamevaa magunia haa hivyo mshiriki kutoka Kilimanjaro aliwatoa nje na
kuibuka mshindi.
Mambo
yalizidi noga zaidi ambapo washiriki waliendelea kutoa Burudaani ya
nguvu kwa wanakijiji wa Kijiji cha Kisanga ambapo hapa sasa Caroline
Chilele(Morogoro) , Eva Daudi (Pwani) na Dina Sumari (Meru) walichuna
vikari wakiwa wanatembea kwa mwendo wa kasi huku wakiwa na vijiko nyenye
ndimu Mdomoni..Hata hivyo mshindi ilikuwa ni lazima apatikane na
Calorine alifanikiwa kuibuka kidedea
Ulizani
washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula hawawezi kuziburuta
Njinga.... Ilikuwa ni Burudani zaidi hapa ambapo sasa Hawa Mkata(Mtwara)
,Edna Kiogwe (Dar es salaam), na Upendo Mhomisoli (Njombe)
walishindana vikali kuendesha Baiskeri. Hata hivyo Mshiriki toka Mtwara
aliibuka Mshindi
Siku
hii kwa hakika wanakijiji walishuhudia Burudani ya kipekee na ya aina
yake kabisa, hapa wakina mama hawa walikuwa wanajikumbusha enzi za utoto
wao ambapo walicheza ule mchezo Maarufu sana uitwao Reje hapa
walidunguana, walitoa kijasho maana shughuli ya kukwepa Mpira si ya
masihala, Calorine Chilele(Morogoro) aliibuka Mshindi.
Na
Mwisho Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Shindano
linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na
kurushwa katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30
Jioni na Kurudiwa saa 11:30 asubuhi ambapo hapa ilikuwa ni vuta ni
kuvute mpaka kieleweke hapa washiriki wote walikuwa wanashindana kwa
kasi ya ajabu sasa kilichotokea hapa ni cha kushangaza kamba ilikatika
hivyo kukawa hakuna mshidi wakatoka sale sale..
0 Comments