Bi.
Bahati Muriga alifika Ubalozi wa Tanzania, Washington DC
kuhudhuria tafrija iliyoandaliwa na Oxfam America. Bi. Muriga aliongelea
maisha yake katika Mkoa wa Mwanza alipokuwa anafanya kazi kama Mkuu wa
shule ya msingi, pamoja na hayo pia aliweza kuingia katika shughuli za
kilimo akitafuta kipato ya kusomesha watoto wake wawili ili kuwapatia
maisha bora.
Ubalozi
wa Tanzania Washington DC ulipata ugeni wa wasau kutoka mashirika
mbalimbali waliokuja kuungana na Oxfam America inayoandaa Siku ya
Chakula Duniani “World Food Day 2015” tarehe 16 Octoba. Bi. Muriga
atasafiri kwenda katika mji wa Des Moines, Iowa kushiriki katika ziara
na Oxfam inayoandaa matamasha mbalimbali kama ya “World Food Prize”.
Bi
Bahati Muriga akielezea ni jinsi gani alivyo na furaha kufika ubalozini
na kuweza kukutana na watu mbalimbali kutoka mashirika tofauti hususan
OXFAM.
Bi Bahati Muruga akiwa pamoja na mwenyeji wake wa jioni hiyo Afisa ubalozi Suleiman Saleh.
Wageni
mbalimbali waliweza kuhudhuria na kuchanganyika pamoja na wenyeji wao
ambao ni wafanyakazi wa ubalozi Pichani ni Mayor Mlima pamoja na Alice .
No comments:
Post a Comment