Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka kushoto)akiwa
ameshikana mikono na baadhi ya viongozi wa taasisi zilizowezeshwa na
Kampuni hiyo kufanya wanajamii maisha yao kuwa murua.Wakati wa hafla ya
Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni hiyo ya“Life is better” inayolenga
kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi kwa kutuma
na kupokea pesa kwa M PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto katika picha Msimamizi wa
kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts,Mmoja wa akina mama aliyepona
Fistula Cherry Msangi,Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya
CCBRT,Brenda Msangi na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto)akijadiliana jambo na
Mkurugenzi wa walemavu wa hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi wakati wa
hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni hiyo “Life is better”
inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi
na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi
,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa akina mama aliyetibiwa na kupona Fistula katika hospitali ya CCBRT,
Cherry Msangi akitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi
wa kampeni mpya ya Vodacom Tanzania ya” Life is better” inayolenga
kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma
na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam,Wengine katika picha ni Msimamizi wa
kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts na Mkurugenzi wa walemavu katika
Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi(kulia).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na waandishi wa
habari pamoja na wadau mbalimbali(hawapo pichani)wakati wa hafla ya
Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya “Life is better inayolenga
kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma
na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom
Tanzania, Ian Ferrao(hayupo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa
kampeni mpya ya kampuni hiyo ya “Life is better inayolenga kuendelea
kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na
kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi ,Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao amezindua kampeni mpya ya kampuni
hiyo inayojulikana Kama ‘Life is Better,’katika hafla iliyofanyika
jijini Dar esk Salaam.Kampeni hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani
Vodacom imeweza kuleta mabadiliko kwenye jamii ya watanzania tangu ianze
kutoa huduma nchini, pamoja na mafanikio hayo mwaka 2016 imejizatiti
kuendelea kuleta mabadiliko makubwa kwa kuipeleka Tanzania katika
ulimwengu wa sayansi na teknolojia,”alisema Ferrao na kuongeza kuwa
kampuni inajivunia kutoa huduma za maongezi na intanet yenye kasi kubwa
ambazo zinawezesha wateja kuzitumia kubadilisha maisha yao na kubuni
fursa mpya.
Ikiwa
ni kampuni inayoongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa nchini mwaka wa 2015
imepata mafanikio makubwa kwa kuanzisha huduma mbalimbali ambazo
zimegusa maisha ya watanzania wengi katika kuzitumia na zinazidi
kuwarahishia maisha na zimewawezesha kuingia katika ulimwengu wa
teknolojia.
“Mwaka
huu umekuwa wa mafanikio makubwa ambapo Vodacom imeweza kubuni huduma
za kuboresha maisha ya wateja wetu kupitia mawasiliano na hii imetokana
na mkakati wa kampuni wa kuwekeza katika miundombinu ya
mawasiliano,wafanyakazi wake na kwenye ubunifu wa kiteknolojia na ndio
maana imeweza kuanzisha huduma mbalimbali za kuwarahisishia maisha
wateja wake ambazo wanaendelea kuzifurahia”.Alisema
Hadi
sasa, Vodacom imewekeza dola za Marekani bilioni moja, na imejenga
mtandao wa kutoa huduma za intaneti za 2G na 3G unaowafikia asilimia 87
ya Watanzania nchini kote na imeongeza idadi ya wateja wake kufikia
ziadi ya milioni 12.
Alisema
mwaka wa 2015 ulianza kwa Vodacom kuanzisha promosheni kubwa ya
JayMillions iliyokuwa inatoa nafasi ya washiriki kujishindia hadi
shilingi milioni 100 kwa siku na wateja walioshiriki na kushinda maisha
yao yamebadilika na kuwa bora na kufanikiwa kutimiza ndoto zao .
“Promosheni
ya JayMillions imebadilisha maisha ya washindi kwa ndoto zao
kutimia,wapo ambao wameendeleza biashara zao,wapo ambao wamejiendeleza
kielimu,wao waliojenga nyumba na kuanzisha biashara.Tunajivunia
kushiriki katika hatua ya kubadilisha maisha yao kutokana na zawadi za
fedha walizojishindia kupitia promosheni hii.”Alisema Ferrao.
Mafanikio
mengine ya kampuni aliyabainisha kuwa ni kuzidi kukua kwa Huduma ya
M-Pesa inayotumiwa na watanzania zaidi ya wateja milioni 7 nchini na
ikiwa na mtandao wa mawakala zaidi ya 85,000 nchini kote imevuka mipaka
ya nchi kwa ushirikiano na Kampuni za Safaricom ya Kenya na MoneyGram
ambapo hivi sasa mteja anaweza kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya
nchi kupitia huduma hii,vilevile huduma ya kujiwekea akiba na kukopa kwa
urahisi kupitia simu ya mkononi ya M-Pawa imezidi kuimarika,kuaminiwa
na kutumiwa na wateja wengi.
“Zaidi
ya wateja milioni 1.5 wanatumia huduma hii wakiwa wameweka akiba
inayofikiashilingi bilioni 6.8 na mikopo inayofikia milioni 500
inatolewa kwa wateja,huduma imechangia kuwezesha watanzania wengi kuweza
kupata huduma za kibenki”.Alisema.
Huduma
zinginezo ambazo zimeanzishwa na kuendelea kufurahiwa na watumiaji wake
baadhi yake alizitaja kuwa ni kampeni ya RED,Spend and Get.Huduma ya
RED inawarahishia maisha wateja wenye shughuli nyingi ambapo wanapata
kifurushi maalumu na kupata huduma zote za mawasiliano kwa gharama nafuu
na M-Pesa wakati huo huo wanajipatia ofa ya kurejeshewa asilimia
10%kupitia akaunti zao za M-Pesa.
Vilevile
alizitaja huduma za kuleta furaha na burudani kwa wateja kama vile
Ishi Kistaa na Mziiki ambazo zinawawezesha wateja kusikiliza muziki
kutoka kwa wasanii mbalimbali kupitia simu zao za mkononi na kuhusu
michezo kampuni inaendelea kuwa mdhamini wa ligi ya soka nchini.
Pia
aliitaja huduma ya Kilimo Klub ambayo imelenga kuboresha maisha ya
wakulima na kuongeza uzalishaji ambapo wakulima wengi hususani wanaoishi
vijijini wanaendelea kuifurahia kwa kuweza kupata mikopo yenye
masharti nafuu ya M-Pawa ambayo hasa imewalenga wao ikiwemo kupata
taarifa za hali ya hewa na bei za mazao kwenye masoko. “Vodacom
itaendelea kufanya ubunifu wa huduma za aina mbalimbali ambazo
zitawarahishia maisha zaidi na kuwafikia watumiaji wengi wa simu za
mkononi tofauti na sasa ambapo wapo baadhi hawazipati”.Alisema
Vilevile
alibainisha kazi kubwa iliyofaywa na taasisi ya kuhdumia masuala ya
kijamii ya Vodacom Foundation katika kuleta mabadiliko kwenye jamii
ambapo kwa mwaka huu ilijikita zaidi kutoa misaada mbalimbali kwa jamii
nchini kote hususani kwa upande wa elimu , afya na makundi mbalimbali
yenye mahitaji.
Mwaka
huu imewezesha operesheni kwa ajili ya wanawake 1,000 walioathirika na
fistula, kuwezesha wasichana kubaki shuleni kupitia mradi wa Hakuna
Wasichoweza ,kusaidia wahanga wa ugonjwa Sickle Cell,Saratani,huduma ya
uzazi kwa akina mama ya ‘Wazazi Nipendeni,kuendesha kampeni za Usalama
barabarani na kuwezesha zaidi ya wanafunzi kusoma elimu ya kompyuta kwa
vitendo mashuleni,kufadhili kituo cha MABINTI kinachotoa mafunzo kwa
wanawake waliopona ugonjwa wa Fistula “Dhamira yetu kubwa ni kuona
tunatokomeza ugonjwa wa Fistula nchini na kukabuliana na changamoto
mbalmbali zilizopo katika sekta ya afya na elimu”.Alisema.
Mwaka
huu umekuwa wa mafanikio na Vodacom imeweza kubadilisha maisha ya
maelfu ya watanzania kuwa bora na imejizatiti na kujipanga kupitia
kampeni hii ya Life is Better kuendelea kufanya vizuri mwakani lengo
kubwa likiwa ni kutimiza dhamira yake ya kubadilisha maisha ya
watanzania kupitia teknolojia na kuwapeleka watanzania katika ulimwengu
wa sayansi na teknolojia.
Katika
mwaka ujao itaendelea kubuni huduma mbalimbali za kuboresha maisha ya
watanzania kupitia teknolojia ikiwemo kuwawezesha watanzania wengi
kuunganishwa na huduma za internet na kuwadhihirishia jinsi huduma hii
ni ya msingi kwa kubadilisha maisha ya watu na kujenga Tanzania iliyo
bora katika miaka ijayo.
0 Comments