Benki ya DCB COMMERCIAL imetoa madawati 100 kwa shule ya msingi Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi yake ya kuchangia madawati 300 kwa shule za manispaa tatu za mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba
akizungumza na waanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es
Salaam leo amesema kuwa benki ya DCB imeguswa na tatizo la ukosefu wa
madawati kwa shule ya msingi hapa nchini.
Amesema kuwa bodi na uongozi wa benki ya DCB inaunga mkono juhudi za
serikali katika kukabiliana na tatizo la madawati hapa nchini inetoa
madawati 100 katika shule ya Msingi Lubakaya jijini Dar es Salaam leo.
Nae Mkuu wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya
Zingiziwa, Said Chitumba amewashukueu benki ya DCB kwa mchango wao kwa
kutoa madawati 100 katika shule hiyo ikiwa shule hiyo inavyumba 16 vya
madarasa na sasa wanaukosefu wa madawati 300.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa
madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba
jijini Dar es Salaam leo, madawati ambayo yatapelekwa katika shule Mpya
ya Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa madawati na Mkuu
wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakimkabidhi
madawati Mkuu wa Shule ya Msingi, Lubakaya (Katikati) jijini Dar es
Salaam leo. Katika Hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam leo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na
majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa wamekaa kwenye madawati
mara baada ya kukabidhi madawati kwenye shule ya Msingi Lubakaya iliyopo
kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam leo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko madawati na Mkuu wa
kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa wamekaa
kwenye madawati na wanafunzi wa shule ya Msingi Mnazi Mmoja
wakiwawakilishi wanafunzi wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam leo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na
majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa kwenye picha ya pamoja na
viongozi mbalimbali wa shule na wa serikali katika picha ya pamoja mara
baada ya kukabidhi madawati 100 kutoka benki ya DCB jijini Dar es Salaam
leo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza katika Hafla Fupi ya Kuwakabidhi madawati 100 ya shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa, Said Chitumba
akiwashukuru Benki ya DCB akiwashukuru benki ya DCB mara baada ya
kukabidhiwa madawati 100.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kabla ya hafla fupi ya
kusherekea miaka 19 ya benki hiyo na kuzindua wa huduma tatu za benki
hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Hatari David Lusala, kulia ni Mkuu wa Rasilimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
Meneja Operesheni wa Benki ya Exim, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Kadi
za malipo za Exim (TANAPA cards, Master cards and VISA cards) ambazo
zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA. Kadi
hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki na pia kuzuia upotevu
wa mapato katika tasnia ya Utalii. jijini Dar es Salaam leo. Kushoto
ni Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga.
Mkuu
wa Kitengo cha hatari wa Benki ya Exim, David Lusala (Katikati)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha uhasibu, George Binde.
Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga akikata utepe kuzindua huduma ya Mfumo
wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza
uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Raslimali watu wa benki ya Exim, Fredrick Kanga akionesha bango la huduma ya Mfumo
wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza
uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi
wa Benki ya Exim wakiwasha mishumaa kwenye keki kusherekea miaka 19 ya
benki hiyo hapa nchini jijini Dar es Salaam leo.
BENKI
ya Exim Tanzania imesheherekea kuadhimisha miaka 19 ya ukuaji na
uvumbuzi kwa kuzindua huduma mpya tatu kwa wateja wake jijini Dar es
Salaam leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha
Fedha wa Benki ya Exim, Selemani Mponda amesema kuwa leo wanasherekea
miaka 19 tangu kuwepo hapa nchini ikiwa na mafanikio makubwa Katika
miaka 19, benki hiyo imejenga utendaji bora na imara katika fedha
wakiwa na rasilimali zenye thamani ya TZS 1.5 Trilioni kufikia Juni
2016.
Amesema
kuwa Faida kabla ya kodi katika kipindi cha pili cha mwaka ilikuwa
shilingi bilioni 64 na pia wameweza kuwa na wastani wa ukuaji kwa mwaka
wa asilimia 30.
Mafanikio
ya benki ya Exim Tanzania ni kuweza kuwa na makao nchini Uganda kwa
kununua benki ya Imperial ya Uganda mapema mwaka huu. Benki ya Exim sasa
ina hisa za asilimia 58.60 katika taasisi hiyo mpya ambayo inayofanya
biashara kama Benki ya Exim Uganda. Wakati ikijikita kuwa benki ya
kikanda tayari ina matawi 43 katika nchi nne zikiwemo Tanzania, Uganda,
Djibouti na Comoro na pia ikiwa na mipango ya kuendelea kujitanua katika
masoko mengine katika miaka mitano ijayo.
Amesema kuwa huduma zilizozinduliwa ni:-
1.
Uwezo wa kutoa taarifa za udanganyifu katika kampeni ya kupambana na
udanganyifu ikiwa na lengo la kutengeneza mazingira ya kutokuwa na wizi
katika tasnia ya benki.
2.
Kadi za malipo za Exim (TANAPA cards, Master cards and VISA cards)
ambazo zinaweza kutumika katika Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA.
Kadi hizi zitaboresha huduma ya malipo ya kielektroniki na pia kuzuia
upotevu wa mapato katika tasnia ya Utalii.
3. Mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika ambao utaongeza uwezeshaji wa wafanyakazi kwa kiasi kikubwa.
Katika
miongo miwili iliyopita, ukuaji wa benki hii na mchango wake wa kiuc
humi na kijamii umetambulika sio tu katika Tanzania bali pia katika
kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa sababu ya ubora katika
utendaji wake.
0 Comments