Pamoja
na kuwepo kwa maendeleo ya kasi katika nyanja mbalimbali lakini sekta
ya teknolojia inabaki kuwa moja ya njia ambayo imechangia kwa kiasi
kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo kwa kurahisisha kazi nyingi
kufanyika kwa haraka.
Kwa
kutambua hilo, kampuni inayohusika na utoaji wa huduma zinazohusiana na
teknolojia ya EnGenius imeingia katika makubaliano na kampuni ya
usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia ya Red Dot ili iweze kusambaziwa
vifaa na huduma mbalimbali ambazo zinafanywa na Red Dot katika nchi za
Afrika Mashariki.
Mkuu
wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao akizungumzia kazi ambazo wanazifanya na
mipango ya kutoa bidhaa bora kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kampuni
ya EnGenius ambayo inatoa huduma kama za internet wireless, radio
frequency (RF) technology na kusambaza bidhaa mbalimbali kama kompyuta
imesema kuwa imefanya maamuzi ya kuingi katika makubaliano na Red Dot
ikiamini kuwa ni moja ya njia sahihi ambayo itawawezesha kuwafikia
wateja kwa karibu zaidi.
Akizungumzia
makubaliano hayo, Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao alisema kampuni
ao kwa sasa inahitaji kujitanua katika nchi za Afrika Mashariki kama
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia hivyo wameungana na Red Dot
ili waweze kukuza biashara yao zaidi.
"Tumeingia
makubaliano na moja ya wasambazaji wakubwa wa Red Dot na tunaamini
watatusaidia EnGenius kufikia malengo yetu ya kuwa wauzaji wakubwa wa
bidhaa za kiteknolojia kwa Afrika Mashariki, tunafahamu kuwa ni
wasambazaji wakubwa na atatusaidia kukuza biashara yetu," alisema Hsiao.
Na Rabi Hume, modewjiblog.com
Mkurugenzi
Mtendaji wa Red Dot Distribution akielezea jinsi ambavyo wamejipanga
kufanya kazi na EnGenius. (Picha zote na Na Rabi Hume, modewjiblog.com)
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani alisema
kuwa ni ushirikiano mzuri ambao wameanza kuufanya na EnGenious na wana
mipango mingi kuhakikisha malengo ambayo yamewekwa yanafikiwa.
"Tuna
taraji mafanikio makubwa, Red Dot ni kampuni ya kitanzania ambayo
inafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki kwahiyo tunatazamia
ushirikiano huu utakuwa na faida," alisema Bharwani.
Meneja
Mkuu wa Red Dot Distribution Tanzania, Rajesh Adiani akifungua halfa ya
uzinduzi wa makubaliano kati ya Red Dot na EnGenius kwa kuelezea
shughuli ambazo wanazifanya.
Mkurugenzi
wa Mauzo na Masoko wa EnGenius, Alishan Zaidi akilelezea huduma ambazo
wanazitoa za kiteknolojia na usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia kama
kompyuta na kamera za usalama.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani na Mkuu wa Kanda wa
EnGenius, Van Hsiao wakipongezana baada ya kuingia rasmi katika
makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia bidhaa ambazo zinatolewa na EnGenius.
Baadhi ya wageni waaliakwa waliohudhuria halfa ya makubaliano ya Red Dot Distribution na EnGenius.
0 Comments