Serikali
kupitia Wizara ya Ujezi Uchukuzi na Mawasilano imebariki uzinduzi wa
televisheni mpya ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes Tanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bibi. Maria Sasabo amesema Serikali imefarijika sana na ubunifu kutoka
kwa kampuni ya StarTime Tanzania kwa kuanzisha televisheni ya kidigitali
isiyotumia kinga’muzi kupata matangazo ya channeli mbalimbali.
“Hii
ni fursa kwa watanzania kujipatia televesheni hizi ambazo ziko katika
teknolojia ya hali juu sana ambazo zitasaidia Tanzania kuingia katika
ulimwengu mpya wa mapinduzi ya sekta ya Habari na Mawasiliano” alisema
Bibi. Maria.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao amesema kuwa
StarTimes imelazimika kutoa televisheni hizo za kisasa ili kuendana na
ukuaji wa teknolojia ambapo wateja wataweza vipindi vinavyoenda na
wakati katika ubora wa hali ya juu.
“Tutahakikisha
tunawapa wateja wetu vipindi vyenye ubora na muonekano mzuri ambao
wataufurahia ulimwengu wa Digitali unaoendelea kubadilika kila kukicha
duniani” alisistiza Bw. Liao.
Ameongeza
kuwa televisheni hizo zimetengenezwa katika ubora unaotakiwa na ni
rafiki kwa mazingira na zimezingatia matumizi madogo ya umeme na
zinapatikana kwa bei nafuu ukilinganisha na televisheni kutoka makampuni
mengine.
Televisheni
hizo za kidigitali zinaonesha zaidi ya channeli 100 za kitaifa na
kimataifa kuanzia habari, muziki, michezo, sinema, thamthilia,katuni,
filamu na vipindi vya Dini.
Mshehereshaji
Luvanda akiwakaribisha wageni wakati wa hafla ya uzinduzi wa
televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania
uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao akizungumza wakati wa hafla ya
uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni yake uliofanyika
Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo
akizungumza na wadau sekta ya Habari na Mawasiliano wakati wa hafla ya
uzinduzi wa televisheni ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes
Tanzania uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Meneja
Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania Bw. Juma Sharobaro
akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya kumpata mshindi wa
moja ya televisheni za kidigitali katika hafla ya uzinduzi wa
televisheni hizo uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao(kushoto) akikabidhi zawadi ya
moja ya televisheni za kidigitali yenye upana wa inchi 40 kwa mshindi wa
televisheni hiyo Bw.John Paul wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(kushoto)
akipokea zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao(kulia) wakati wa
hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini
Dar es Salaam.

akikabidhi zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali yenye upana wa
inchi 32 kwa mshindi wa televisheni hiyo Bw.Ambokile Mapasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(
wa pili kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa
kampuni ya Startimes Tanzania jinsi ya televisheni za kidijitali
zinavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo
uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(
wa pili kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa
kampuni ya Startimes Tanzania jinsi ya televisheni za kidijitali
zinavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo
uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao (kulia) akimueleza jambo Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo(kulia)
wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni
ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Wasanii
kutoka Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa
televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania
uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
0 Comments