Kushoto
ni msanii wa Bongo Fleva, G nako na Rayton Kwembe Mkurugenzi wa Nuru
Coffee Chapchap wakizungumza na Wanahabari (Hawapo pichani)
G Nako kuzindua bidhaa bora ya Nuru Coffee Chapchap
Na Mwandishi Wetu, Dar
Es Salaam, April 2017: DMG Tanzania, kampuni tanzu ya chakula na
vinywaji nchini, imezindua bidhaa yenye mchanganyiko wa kahawa, maziwa
na sukari ya “Nuru coffee Chapchap” yenye hadhi ya kimataifa na ladha
thabiti.
Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka kufuatia
changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea nchini ikiwa na dhumuni
la kulenga kila Mtanzania kuonja ladha mpya ya Nuru coffee Chap chap
ikipatikana nchini kote nchini na katika masoko yote.
Kutokana
na ubunifu wa DMG Tanzania unaowatofautisha na wapinzani wake katika
soko, kampuni hii imewawezesha Watanzania hata ya hali ya chini, kuwa na
uwezo wa kuonja ladha murua yenye mchanganyiko wa maziwa, sukari na
kahawa kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh 500=/
Akizungumzia
bidhaa hiyo mpya ,Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa Nuru Coffee Chapchap
anasema “ Nuru coffee Chapchap ni bidhaa ya kipekee na ni moja kati ya
bidhaa madhubuti katika kampuni yetu. Nuru ni neno la Kiswahili
linamaanisha “mwangaza” ikiwa na maana ya asili, Nishati, na matumaini .
Nuru huondoa giza na kuweka dhahiri vitu vilivyofichika. Nuru hung’aa
popote na kurudisha tumaini kwa watu waliokata tamaa.”
Hivyo
uzinduzi wa kahawa ya Nuru coffee Chapchap imekuja kwa wakati muafaka na
kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa za ajira
zinazotolewa nchini na kampuni hii.napia
bidhaa ya nuru coffe imekuwa nuru kwa watanzania kwani imewawezesha
kujipatia chai yenye mchanganyiko wa sukari maziwa na kahawa kwa gharama
nafuu kabisa kwa kuzingatia hali yetu uchumi.
“Tunayofuraha
kubwa kuzindua bidhaa hii ya kiwango cha juu itakayokidhi maisha ya
mtumiaji, kwa kumpatia ladha nzuri ya kahawa bora kabisa na chapchap.
Nuru coffee Chapchap inatokana na aina mbili kuu za kahawa nchini,
Robusta na Arabika kwa asilimia 100 na kutengenezwa kwa mchanganyiko
madhubuti wa maziwa na sukari, ili kuleta ladha nzuri ya kuvutia.
Tumejipanga na tuna ujasiri mkubwa juu ya bidhaa yetu mpya na hivyo
hatutatetereka.” Alisema ,Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Hivi
sasa Nuru coffee Chapchap inapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam,
Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Dodoma na Arusha, na pia bidhaa hii
inatarajiwa kupatikana mikoa mingine nchini miezi michache baadae.
Katika
kusherekea uzinduzi wa Nuru Coffee Chapchap katika soko la nchini
Tanzania kampuni ya DMG Tanzania imeandaa kampeni itakayohusisha
supamaketi kubwa mbalimbali kama TSN Supermarkert iliyopo kibo complex,
American Super Markert pugu road na Nakumatt Mlimani City. Kampeni hiyo
pia itahusisha upatikanaji wa nuru Coffee katika mitaa mbalimbali katika
jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 – 25 Aprili mwaka huu.
Kitu
kikubwa Zaidi katika bidhaa ya Nuru coffe ni utaalamu wa usindikaji wa
bidhaaa hiyo na ufungaji wa paketi zake zinazolenga kuibua hisia ya
mtumiaji kabla hata hajainunua.
Nuru coffee Chapchap wafurahia
kumtaja na kumtambulisha George Sixtus Mdemu, (G Nako) ambaye ni
mwanamuziki wa kizazi kipya “maarufu kama Bongo Fleva” kuwa balozi wa
bidhaa ya Nuru Coffee Chapchap nchini Tanzania. G Nako atakuwa
akiitangaza bidhaa ya Nuru coffee Chapchap katika soko la Tanzania
pamoja na vyombo vya habari kama radio, TV, magazeti na mitandao ya
kijamii.
Pamoja na mambo mengine G Nako kama balozi
wa Nuru coffee Chapchap atakuwa akishirikiana pamoja na wateja wetu
kueneza bidhaa yetu yenye ubora wa hali ya juu.
“Tunayo
furaha kubwa na tunategemea G Nako ataeneza uwezo wa bidhaa yetu na
kuwa balozi madhubuti. Tunajivunia kazi tunayoendelea kufanya pamoja
naye na tunategemea kuimarisha uhusiano wetu kwa kuikuza lebo yetu na
kuieneza kote nchini” Alisema Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa kampuni
hiyo.
“Mimi pamoja na Nuru coffee Chapchap tumekuwa
na uhusiano thabiti, DMG Tanzania ni kampuni nzuri na ninajivunia
kufanya kazi pamoja nayo, “ G Nako.
DMG Tanzania
haitabaki nyuma katika kuhakikisha inaongeza ubora katika bidhaa yake ya
Nuru coffee Chapchap na pia inampango wa kuzindua bidhaa nyingine
nyingi chini ya mwamvuli wa lebo ya Nuru. Ikiwa na lengo la kukuza
usambazaji wa bidhaa yake DMG Tanzania inalenga kuifikia Tanzania yote
pamoja na Africa Mashariki.
KUHUSU DMG
DMG
Tanzania inadhamira ya kubadili hali ya sasa ya Tanzania ikiwa ni kukuza
ushirikiano wa kibiashara. Tuna lengo dhabiti la kujifunza kutoka nchi
nyingine kama Korea ili kupata uzoefu wa kiteknolojia na kupata ujuzi
ili kujenga undugu na ushirikiano hapa Tanzania.
Tumedhamiria kusambaza kahawa nzuri na yenye kiwango kizuri cha kahawa, maziwa na sukari ili kuleta ladha mpya kwa watumiaji.
Nuru
coffee Chapchap ina gramu 120 (12g × 10pks) ikiwa na mchanganyiko kama
ifuatavyo:- kahawa 5.5%, sukari, Nondairy cream [glucose syrup,
hydrogenated oil palm, sweet whey powder, sodium caseinate, potassium
phosphate], dextrin, silicon dioxide, nature identical hazelnut flavor
Kwa
sasa Nuru coffee Chapchap inazalishwa nchini Korea ya Kaskazini ingawa
tunategemea kwa siku za karibuni iwe inazalishwa hapa nchini.
DMG
Tanzania inadhamira ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha masoko yote na
baadae kuenea sehemu nchi zote za jirani ikiwa ni pamoja na ukanda wa
mashariki kati na kusini mwa Afrika. Pia DMG Tanzania inalenga
kuitangaza Nuru coffee chapchap ili kufikia lebo kubwa zaidi nchini
Tanzania.
Arusha Publicity Provides best quality branding services in Strategy and Development, Identity Design, Messaging and Communication, Marketing and Promotion, Measurement and Analysis.
Providing best quality branding services in Strategy and Development, Identity Design, Messaging and Communication, Marketing and Promotion, Measurement and Analysis.
Wazalendo 25
Fashion Blogger
Providing best quality branding services in Strategy and Development, Identity Design, Messaging and Communication, Marketing and Promotion, Measurement and Analysis.
Judy Mwaheleja
Blogger
Providing best quality branding services in Strategy and Development, Identity Design, Messaging and Communication, Marketing and Promotion, Measurement and Analysis.
Khadija Kalili
Entertainment Blogger
Providing best quality branding services in Strategy and Development, Identity Design, Messaging and Communication, Marketing and Promotion, Measurement and Analysis.
0 Comments