BENKI YA DTB, EFM RADIO WATOA MSADA WA MADAWA TAASISI YA MIFUPA MOI



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dkt.Respicious Boniface, (kulia), akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Meneja wa Benki ya DTB Tawi la Morocco jengo la Airtel, jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena .Y. Sinare, kwenye jengo jipya la MOI, leo Juni 18, 2017. DTB kwa kushirikiana na EFM Radio, wametoa msada wa madawa mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo

Dkt. Boniface, akipokea sehemu ya msada wa madawa kutoka kwa Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Jesca Mwanyika kwenye jengo jipya la MOI jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2017. EFM kwa kushirikiana na Benki ya DTB wametoa msada huo wa madawa yenye thamani ya shilingi milioni 4 ili kusaidia watoto wenye matataizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo

Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama Aunt FIFI, akikabidhi sehemu ya msada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Precious Boniface



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI ya DTB kwa kushirikiana na EFM Radio kupitia kipindi chake cha “Bustani ya Watoto”, wametoa msada wa madawa mbalimbali kwa Taasisi ya Mifupa MOT iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo Juni 18, 2017.


Akikabidhi madawa hayo, Afisa Uhusiano wa EFM Radio, Bi.Jesca Mwanyika alisema, EFM kupitia kipindi chake cha watoto cha “Bustani ya Watoto” iliamua kuwashirikisha DTB ili kuona ni namna gani wanaweza kusaidia watoto waliolazwa kwenye Taasisi ya MOI hususan wale wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.


“Sisi kama EFM Radio tuna kipindi cha watoto cha Bustani ya Watoto, tumeona kwa vile tunashughulika na watoto, na kwa vile siku chache zilizopita Dunia iliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika Duniani, basi tumeona tutoe kiasi hiki cha madawa kuwasaidia watoto hawa wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa hapa MOI.”Alisema Bi. Jesca.


Akizungumza kwa niaba ya DTB, Afisa Masoko wa benki hiyo, Bw.Baguma Ambari alisema, Benki kama taasisi inayotoa huduma kwa wananchi, inao wajibu mkubwa kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii na hivyo imefurahishwa kuungana na EFM Radio katika kutoa msada huo wa madawa ambao anaamini utasaidia katika kuwahudumia watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.


Akitoa shukrani zake, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alisema, msada huo wa madawa utasaidia sana katika kuwapatia huduma za afyan watoto hao. “Kama mjuavyo wengi wa watoto hawa hutoka kwenye familia masikini kwa hivyo msada huu wa madawa utasaidia sana katika kuwapatia huduma.


“Madawa haya ni anti-biotic pamoja na kwamba watoto hawa wanaletwa hapa wakiwa na matatizo ya vichwa baadhi yao huwa na infection sehemu mbalimbali za miili kama vile vifua au tumboni, lakini pia husaidia kutibu vidonda n.k.” Alifafanua Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface (mbele) akiongozana na Meneja wa DTB Tawi la Morocco jijini Dar es Salaam, Bi.Sheena Y. Sinare, wakati wakitembelea kuwajulia hali watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa kwenye taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es Salaam

Dkt. Boniface (kushoto), akizungumza jambo na Bi. Sinare wakati walipokuwa kwenye moja ya wodi za watoto hao
Dkt. Boniface (kushoto), akizungumza jambo na Bi. Sinare wakati walipokuwa kwenye moja ya wodi za watoto hao kuwajulia hali


Afisa Masoko wa DTB, Bw. Baguma Ambar(kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msada huo. Kulia ni Kaimu Afisa Uhusiano wa MOI, Bw.Frank Matua

Afisa Masoko wa DTB, Bw. Baguma Ambar, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kutoa msada huo.

Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama Aunt FIFI,akielezea kilichomsukuma kuwa na mpango huo wa kutoa msada

Mtayarishaji wa kipindi cha "Bustani ya Watoto" kinachopeperushwa na EFM, ambaye ndiye chachu ya kutolewa kwa msada huo, Bi. Flora Amon maarufu kama Aunt FIFI,akielezea kilichomsukuma kuwa na mpango huo wa kutoa msada. Kulia anayesikiliza kwa makini, niAfisa Uhusiano wa EFM, Bi. Jesca Mwanyika

Dkt. Boniface akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msada huo

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msada huo

Baadhi ya wafanyakazi wa EFM na DTB waliohudhuria hafla hiyo

Baadhi ya wafanyakazi wa EFM waliohudhuria hafla hiyo

Mfanyakazi wa EFM, Bw.Sali Mlindila, akiwa amebeba boksi lenye dawa zilizotolewa msada kwa MOI

Wafanyakazi wa EFM na DTB wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alipokuwa akielezea umuhimu wa jamii kuwasaidia watoto hao.

Wafanyakazi wa EFM na watoto wao na wale wa DTB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface

No comments:

Post a Comment

Pages