MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA "WEKA AKIBA NA USHINDE"



Meneja wa Tawi la Samora la Benki ya Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia Ndongole, (kushoto), akimkabidhi IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya “Weka akiba na ushinde” inayoendeshwa na benki hiyo.Hafla hiyo imefanyika leo Julai 18, 2017 kwenye tawi lam benki hiyo Mtaa wa Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wengine ni washindi kutoka kulia, ni Bw. Benester Lazaro na Bi. Grace Machemba wote kutoka Dar es Salaam.







NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


WATEJA wanne wa Mwalimu Commercial Bank PLC wamejishindia zawadi za IPAD na vocha za manunuzi baada ya kuibuka washindi kwenye Droo iliyochezeshwa na benki hiyo kufuatia kweney promosheni ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.


Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 18, 2017 wakati wa kukabidhi zawadi za washindi, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, (pichani juu), alisema, Droo hiyo ilikuwa wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na benki kwa kufungua akaunti kwa kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.


Akifafanua zaidi Bw. Lutenganya alisema, kampeni hiyo ilizinduliwa Mei 18, 2017 na wamepokea wateja wengi ambao walishiriki kwenye Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha, (Gaming Board of Tanzania).












Aliwaja washindi hao kuwa ni pamoja na Bw. Shukuru Sanga, kutoka Waning’ombe mkoani Njombe ambaye alijinyakulia IPAD, wakati Bw. Benester Lazaro, na Grace Machemba kutoka Dar es Salaam, walijinyakulia vocha za manunuzi kama ilivyo kwa Bi. Joyce Sangusangu kutoka mkoani Dodoma.


Akifafanua zaidi jinsi kampeni hiyo ilivyoendeshwa, Bw. Lutenganya alisema, kadiri mteja alipoweka akiba zaidi ndivyo alivyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi na amewataka wateja na wananchi wengine kuweka akiba kwani droo nyingine itachezeshwa baadaye mwezi huu.


Aidha alisema hudma za benki hiyo, ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba.


Alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na nafuu, nakuwahakikishia wateja na wananchi kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani benki inatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu ikiwemo huduma ya ATM kwenye mtandao mpana wa UMOJA switch wenye ATM zaidi ya 200 kote nchini.


“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.

Bw. Lutenganya akiwa na maafisa wa benki hiyo wakati akizungumzia zawadi hizo

Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.

Wafanyakazi wa MCB wakiwa kwenye hafla hiyo.

Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niabaya washindi wenzake. Kushoto ni Afisa Mikopo wa benki hiyo, Bw.Isaya Hagamu.

Mshindi wa IPAD, Bw. Shukuru Sanga kutoka Waning’ombe mkoani Njombe, akiongea kwa niaba ya washindi wenzake.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, cha benki ya Walimu Tanzania, (Mwalimu Commercial Bank Plc-MCB), Valence Lutenganya, (kulia), akizungumza mbele ya washindi wa promosheni ya kwanza ya “weka akiba na ushinde” kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, Julai 18, 2018. Wateja wane wa benki hiyo walijishindia IPAD na Vocha za manunuzi, baada ya kuingia kwenye droo iliyowaibua kuwa washindi. Kwa mujibu wa Lutenganya, mshindi ni lazima aweke akiba si chini ya shilingi elfu 50,000 au kufungua alkaunti na kuweka kiasi hicho cha akiba na hivyo kuingia kwenye promosheni hiyo moja kwa moja. Kutoka kushoto ni Meenja wa tawi la benii hiyo, Leticia Ndongole, Mshidni wa IPAD, Shukuru Sanga, Grace Machemba, (Voucher), and Benester Lazaro, also he won a voucher.

Afisa Mikopo wa MB, Bw. Isaya Hagamu, (kushoto), akimkabidhi zawadi ya vocha ya manunuzi, mshindi wa promosheni ya "Weka akiba na ushinde" inayoendeshwa na benki hiyo, Bw. Benester Lazaro wa jijini Dar es Salaam hukuMeneja wa tawi la Samora la benki hiyo, Bi. Leticia Ndongole, akishuhudia.

Bw. Lutenganya(kulia). akimpongeza Bw. Lazaro kwa ushindi. Kushoto ni Bi Leticia Ndongole

Bi Leticia Ndongole(kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPD, Bw. Sanga.

Meneja wa Tawi la Benki wa Mwalimu, (Mwalimu Commercial Bank, Plc), Leticia Ndongole, (katkati), akishuhudia jinci Meneaj wa Huduma kwa wateja wa tawi hilo, Flora C. Mbogo, (kushoto), akimkabidhi vocha ya manunuzi mteja wa benki hiyo, Grace Machemba, baada ya kuwa mionhoni mwa washindi wa promosheni ya weka akiba na ushinde ya benki hiyo. Hafla ya kukabidhi zawadi hizo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam Julai 18, 2017. Ambapo washindi wengine waliibuka na IPAD na vocha.

Mwanahabari akiwa kazini akitekeleza majukumu yake wakati wa hafla hiyo.

Post a Comment

0 Comments