Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na
Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Mikoa na Halmashauri nchini
kabla ya kutoa Tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika
kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Bibi. Sihaba
Nkinga akizungumza na Maafisa maendeleo ya Jamii katika siku ya ufungaji
wa Mkutano wa 12 wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii na
kuwasisitiza kuwajibika na kujituma katika kuleta maendeleo katika
maeneo yao.
Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Bi. Mwajuma
Magwiza akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) na kuahidi kutekeleza
maelekezo yote yaliyotolewa katika Mkutano huo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akimkabidhi tuzo kwa
Afisa Maendeleo ya Jamii Kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Esterine
Sephania kwa niaba ya Halmashauri ya Kigamboni iliyoibuka kinara wa
uwezeshaji wanawake kiuchumi kupitia mchango wa asilimia 5 katika mfuko
wa maendeleo ya wanawake.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(katikati) na Katibu
Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Bibi. Sihaba Nkinga(wa
tano kushoto mstari wa chini) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa
Maendeleo ya Jamii kutoka katika Mikoa na Halmashauri nchini, mara baada
ya kufungwa kwa Mkutano wa 12 wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya
Jamii ulioambatana na utoaji Tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya
vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi. Picha na Kitengo cha
Mawasiliano WAMJW
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Halmashauri
ya Wilaya ya Kigamboni imekuwa kinara wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
katika vikundi vya uzalishaji mali katika halmashauri zao.
Hayo
yamebainika katika utoaji wa tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya
vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi katika kwa kutenga asilimia
tano (5) katika Bajeti ya mapato ya Halmashauri katika Mfuko wa
Maendeleo ya Wanawake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi fedha
inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akitoa
tuzo hizo Mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.
Selemani Jafo amewapongeza washindi wote waliofanikiwa kutekeleza mpango
wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwatengea asilimia 5 katika
Bajeti ya mapato ya halmashauri.
Ameongeza
kuwa njia pekee ya kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda ni
kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani wengi wao wanashiriki katika
shughuli za kijasilia mali ambazo zinawapa uwezo wa kuanzisha miradi ya
uzalishaji mali na uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo.
Mhe.
Jafo amesisitiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kujituma katika maeneo yao
na kuleta mabadiliko kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika
shughuli za kujiletea maendeleo kufikia uchumi wa viwanda.
Naye
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bibi. Sihaba
Nkinga amesema kuwa Serikali imedhamilia kuwawezesha wanawake kiuchumi
na wao kama wasimamizi wa Sera watahakikisha wanafuatilia utekelezaji
wake katika ngazi za Mikoa na Halmashauri.
“Tumejipanga
kuwawezesha wanawake kiuchumi ambao watasaidia kuiwezesha jamii nzima
kupitia shughuli zao za maendeleo kuelekea kufikia uchumi wa viwanda”
alisema Bibi Sihaba.
Aidha
Bibi Sihaba amewataka maafisa maendeleo kutumia weledi katika kusimamia
uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika ngazi ya halmashauri
kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu katika kushirikiana kuwezesha
wanawake kiuchumi ili kusaidia taifa kufikia azam ya uchumi wa kati na
viwanda .
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri
ya Kinondoni Bi. Mwajuma Mwagiza ameishukuru Serikali kwa kuwezesha
wananchi kiuchumi na kuahidi kuendelea kuhamasisha wanawake kujiunga
katika vikundi vya ujasiliamali ili kuwezesha kuleta maendeleo katika
maeneo yao kufikia uchumi wa viwanda.
Tuzo
hizi za vinara wa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi zimetolewa kwa Mikoa
na Halmashauri kumi zikiongozwa na vinara Halmashauri ya Wilaya ya
Kigamboni itasaidia kuleta chachu ya mabadiliko katika kuwawezesha
wanawake kiuchumi Tanzania.
0 Comments