Kaimu
Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru akimkabithi
gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi na mkazi wa
wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni
ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel,Bi. Jane
Matinde.
Mshindi
wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso
akifungua gari mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara baada ya
kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema
Mwanza. akishuhudia ni Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel David
Wankuru.
Mshindi
wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana Kijiji Gweso
akiwa ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel mara
baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya
Sengerema Mwanza.
Kaimu
Katibu wa Wilaya ya Sengerema Bwana Aaron L Laizer ( wa pili kushoto)
akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi
na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi wa
promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa
Airtel Bi Jane Matinde na Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel
Bwana David Wankuru.
Mkazi
wa wilaya ya sengerma na mvuvi katika kisiwa cha Yozu bwana Kijiji Gweso
Jana amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Airtel yatosha
zaidi.
Akiongea
wakati wa halfa ya kukabithiwa gari lake Bwana kijiji Gweso alisema”
nilipopigiwa simu na Airtel nilipuuzia sikuamini kabisa kama nimeshinda
gari mpaka ndugu zangu waliponipigia na kunihakikishia kuwa mimi
nimetangazwa mshindi ndipo nilipoenda ofisi za Airtel na kukuta kweli
nimejishindia. Mimi ni mvuvi na mke na watoto wawili na nilinunua
kifurushi cha Airtel yatosha cha mia tano tu na furahi sana kushinda
gari hili kupitia promosheni hii”.
“Sijawahi
kumiliki gari hivyo usafiri huu utanisaidia katika shughuli zangu za
uvuvi, za kifamilia na kiuchumi kwa ujumla, nachukua fulsa hii kuwaambia
watanzania wenzangu waamini kuwa Airtel inatoa magari na kwamba wao pia
wanaweza kuwaibuka washindi. Nawashukuru sana Airtel kwa kuboresha
maisha yangu na yawatanzania wengine walioshinda kama mimi”aliongeza
Gweso.
Akiongea
wakati wa kukabithi gari kaimu katibu wa wilaya ya sengerema bwana
Aaron L Laizer alisema” nampongeza sana bwana Kijiji Gweso kwa kuibuka
mshindi, ushindi huu umetuthihirishia wakazi wa sengerema kuwa
promosheni hii ya ya ukweli na zawadi zinatolewa. Tunawashukuru sana
Airtel kwa kutoa huduma bora za mawasiliano nchini ambazo zimerahisisha
shughuli za kiuchumi, kijamii na kiusalama lakini pia kuanzisha
promosheni inayowazawadia wateja wake, na kwa wananchi wa sengerema na
wa mwanza kwa jumla hii nifulsa kwetu tuendelee kutumia huduma za Airtel
na kupata nafasi ya kushinda”.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa kanda ya Airtel Bwana David Wankuru alisema “
promosheni hii bado inaendelea mpaka sasa ni washindi 24
tumeshapatikana , magari bado yapo hivyo natoa wito kwa wakazi wa kanda
yangu na watanzania kwa ujumla kuweza kushiriki. Tunafurahi kuwa na
washindi wane mpaka sasa kutoka katika kanda ya ziwa washindi hawa ni
pamoja na Bi Ester Mathias Mashauri muuguzi bugando, Bi kajala kokutima
said mkulima na mkazi wa bukoba, Seleman Daudi Onesmo mkazi wa nyakato
Mwanza na leo tunamkabithi gari bwana Kijiji Gweso mkazi wa Sengerema’.
Wankuru
aliongeza kwa kusema “kujishindia unatakiwa kujinga na kifurushi
chochote cha Airtel yatosha cha siku, wiki au mwenzi kwa kupiga *149*99#
au kununua vocha ya Airtel yatosha au kwa kununua kupiita huduma ya
Airtel Money, baada ya kununua kifurushi chako namba yako moja kwa moja
itaingizwa kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia gari aina ya
Toyota IST kila siku”.
Promosheni
ya Airtel yatosha Zaidi ilizinduliwa na kampuni simu za mkononi ya
Airtel Mwanzoni mwa mwenzi wa Februari, watanzania wengi kutoka katika
mikoa mbalimbali wameweza kujishindia magari na kubadili maisha ya
kupitia promosheni hii. Magari 24 yameshapata washindi toka promosheni
hii ianze hadi sasa.
0 Comments