Let's Talk Business / Tuongee Biashara Pekee.

Habari Mpya

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, October 14, 2015

BENKI YA NBC YATOA MSAADA KWA WALEMAVU WA NGOZI


 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mussa Jallow (wa tatu kushoto), akikabidhi pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani, katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kuisaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha, Pwani jana. Wengine ni baadhi ya wanachama wa TAS na maofisa wa NBC.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa tatu kushoto) akikabidhi pikipiki kwa mmoja wawakilishi wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha, Pwani jana. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani.
  Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara( NBC) Alina Maria Kimaryo (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanachama wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani  katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha mkoani Pwani jana.
 Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya NBC, Andrew Lyimo (wa pili kulia), akikabidhi baadhi ya misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao ni wanachama wa Chama cha Albino Tanzania (TAS) katika Mkoa wa Pwani. Katika hafla hiyo iliyofanyika Kibaha jana, NBC ilikabidhi msaada wa pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta maalumu ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanachama wa TAS na maofisa wa NBC.
 Meneja Mahusiano ya Biashara wa NBC, Emanuel Mseti (wa tatu Kushoto) akimkabidhi mlemavu wa ngozi, Mwalimu Matimbwa, boksi lenye miwani katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha mkoani Pwani jana. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa NBC na wanachama wa TAS.
 Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo (katikati), akizungumza na mmoja wa walewavu wa ngozi wakati NBC ikikabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu wa wanachama wa Chama cha wenye ulemavu wa ngozi (albino) wa Mkoani wa Pwani. Pamoja na misaada mingine NBC ilikabidhi mafuta maalumu ya ngozi, kofia na miwani vitu vinavyowasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya zinazotokana na hali ya hewa.

Post Top Ad

Your Ad Spot