Benki
ya CRDB inajivunia mapinduzi makubwa katika sekta ya fedha nchini,
iliyoyafanya katika kipindi cha miaka 20 ya uwepo wake, kwa kufanikisha
kuwafikishia huduma za kifedha Watanzania walio wengi na haswa walio
vijijini, hivyo CRDB kujikuta imetimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei,
katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi, katika kutathimini
mafanikio ya benki ya CRDB kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya
Benki ya CRDB.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei, akifanya mahojiano maalum
na Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea, aliyejikita katika kuandika
habari za kimaendeleo, Pascal Mayalla, kuhusiana na maendeleo
yaliyoletwa na CRDB Banki katika kipindi cha miaka 20.
Dr
Kimei amesema, miongoni mwa mafanikio makubwa ya kujivunia ya Benki ya
CRDB, ni kitendo cha benki hiyo kufanikiwa kutimiza malengo, dira na
dhima ya benki hiyo, ambayo ni kufikisha huduma za kibenki kwa
Watanzania wengi zaidi hadi vijijini, ambapo lengo hili limetizwa
kupitia kwa mawakala wa CRDB waitwao Fahari Huduma waliotapakaa nchi
kote hadi Vijijini.
“Katika
mambo mengi ambayo CRDB inajivunia katika miaka hii 20, ni kuingiza
mfumo mpya wa kimapinduzi wa kutolea huduma kwa wateja wetu wengi zaidi
hadi wa hali ya chini ambao wengi wako vijijini, wamekuwa hawafikiwi na
huduma za kibenki, hivyo Lengo na azma ya CRDB ya kuwafikia wateja
wengi, limetimizwa.
Akinamama
wa Kibamba, wakielekea kwenye kituo cha Wakala wa Fahari Huduma wa
Kibamba, kupata huduma za kifedha, wakala huo, unaomilikiwa na Bw. Frank
Mwalinga na mkewe Mainda, wakati wa ziara za kukagua mafanikio ya miaka
20 ya Benki ya CRDB.
Akielezea
mafanikio ya jumla ya CRDB Bank ndani ya miaka ishirini ya kutekeleza
dira, dhima na Mipango Mikakati iliyoshabihiana na dira hiyo, Dr. Kimei
amesema, Mtandao wa CRDB, una matawi 198, unaojumuisha vituo mbadala vya
kutolea huduma kwa wateja zikiwemo ATMs 461, vituo vya Wakala wa Fahari
Huduma 1800, Vituo vya kutoa huduma kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa
40, SACCOs zilizoingia ubia na Kampuni Tanzu ya CRDB Microfinance
Services, 482, na Vifaa vya kutolea huduma kwenye vituo mbalimbali vya biashara kama vile mahoteli, supermarkets, mahospitali 989.
Akizungumzia
mafanikio mengine ya miaka 20 ya CRDB Bank, Dr. Kimei amesema CRDB
Banki ina wateja 1,800,000, wenye amana za zaidi ya shilingi trilioni
4.2. ambapo CRDB Bank imetoa mikopo ya shilingi trilioni 3.3 na kwa sasa
ina jumla ya raslimali za trilioni 5.3.
Pia
Dr. Kimei, amezungumzia baadhi ya huduma ambazo CRDB Bank imekuwa ya
kwanza kuzianzisha, CRDB Bank imekuwa ni benki ya kwanza kuunganisha
matawi yake nchi nzima na kufanya kazi kama tawi moja na hivyo kuwezesha
uhamishaji wa fedha kutoka tawi moja kwenda jingine papo kwa papo tangu
mwaka 1999. CRDB Banki imekuwa ya kwanza kuanzisha mfumo wa kutoa
huduma kwa wateja wake kwa kutumia kadi za ATM mwaka 2002: Hadi leo CRDB
ina kadi za Visa na Mastercard zinazofikia 1,400,000
CRDB
Bank ndio benki ya kwanza kubuni bidhaa inayokidhi mahitaji ya watoto
(Junior Jumbo Account) na wanafunzi (Scholar Account) ambazo leo hii
mabenki yote yameiga. CRDB Bank ndio ya kwanza kuingiza bidhaa mahsusi
ya uwekezaji inayolenga Wanawake—Malkia Account na imekuwa benki ya
kwanza kuona fursa katika kuwapelekea huduma za kibenki kwa watanzania
wanaoishi nchi za nje: Akaunti yenye chapa ya Tanzanite.
Dr.
Kimei amesema haya yote yamewezekana kwa timu ya wafanyakazi 2,682
wanaofanya kazi kwa bidii, ubunifu na kujituma na ari ya hali ja juu.
Akichangia
mafanikio haya ya CRDB, Meneja Mkuu wa CRDB Microfinance Services
Company Ltd, Bw. Sebastian Masaki, amesema CRDB imeyaweza yote hayo
kutokana na juhudi za kuhakikisha inasaidia kupunguza ukosefu wa huduma
za kibenki kwa Watanzania walio wengi, haswa waishio vijijini au mbali
na matawi ya taasisi za kifedha. Hivyo lengo kubwa la CRDB ni kutafuta
njia mbadala za kuwafikishia wananchi huduma za kifedha karibu na mahali
walipo, ndipo ikabuni kuwatumia mawakala wa fahari huduma ambao wako
zaidi ya 1800 na wamesambaa nchi nzima.
Wageni
mbalimbali wakitembelea
Wakala wa Fahari Huduma wa Kibamba, kushuhudia mafanikio ya miaka 20 ya
Benki ya CRDB. wakala huo, unaomilikiwa na Bw. Frank Mwalinga na mkewe
Mainda.
Akinamama
wa Kibamba, wakimpokea kwa furaha, Mkuu Oparations wa CRDB
Microfinance, Bw. Samson Keenja, alipokwenda kutembelea Wakala wa Fahari
Huduma wa Kibamba, unaomilikiwa na Bw. Frank Mwalinga na mkewe Mainda,
wakati wa ziara za kukagua mafanikio ya miaka 20 ya Benki ya CRDB.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya CRDB Micofinance, ambayo ni kampuni Tanzu ya Benki
ya CRDB, Bwana Seabastian Masaki,
akifanya mahojiano maalum na Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea,
aliyejikita katika kuandika habari za kimaendeleo, Pascal Mayalla,
kuhusiana na maendeleo yaliyoletwa na CRDB Banki katika kipindi cha
miaka 20 ambapo kampuni hiyo ya CRDB Microfinance ni moja ya vielelezo
vya mafanikio hayo.
0 Comments