Msanii,
Ally Salehe 'Ali Kiba' akishambulia jukwaa wakati akitumbuiza kwenye
tamasha la kutimiza miaka Miwili ya Chaneli ya Startimes Swahili tokea
kuanzishwa Kwake. Tamasha hilo lililopewa jina la Serebuka Festival
lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jana ambapo
lilidhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.
Msanii, Snura Mushi, akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
Msanii, Juma Kassim 'Juma Nature, akitumbuiza kwenye
tamasha hilo.
Msanii Stamina akipagawisha kwenye tamasha hilo.
Wananchi
wakifuatilia Tamasha la Serebula Festival la kuazimisha miaka miwili ya
chanel ya startimes Swahili iliyoandaliwa na kampuni ya Bluelines kwa
kushirikiana na uwawei jijini Dare s Salaam jana.
Na Dotto Mwaibale
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura Lady Jay Dee na Ali Salehe Ali
Kiba wameonesha umahiri wao wa kuimba kwa kutumia 'live band' katika
tamasha la Serebuka na Festival 2016 lililofanyika jijini Dar es Salaam
jana.
Mashabiki
walioudhuria tamashan hilo walianza kuonesha shangwe baada ya Lady Jay
Dee kupanda jukaani na kuimba tungo na alioimba wimbo wa Ndindindi
mashabiki walilipuka kwa vifijo.
Shangwe
hizo zilidumu hata kwa msanii Ali Kiba ambapo walimtaka aendelee kuimba
licha ya muda wa kuendelea na tamasha hilo kuwa umekwisha.
Ali
Kiba aliwachangua zaidia mashabiki walipoimba wimbo wa Aje ambpo dakika
za mwisho jukwaani hapo akapanda mwanadada na kushuka na msanii huyo na
kuacha mashabiki wakishangilia kwa shangwe.
Wasanii wengine ambao walionesha uhai katika tamasha hilo, Bonivecture Kabobo 'Stamina' ambaye mashabiki walionesha kumuunga mkoano kutokana na aina ya uimbaji wake kuteka mashabiki.
Pia
katika tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya King'amuzi cha Starv
Times liliudhuriwa ma Juma Kasimu 'Juma Nature', Madee,Yamoto Band,
Snura na wengineo ambao waliimba kwa kutumia 'Play Back'.
Tamasha
hilo lililopewa jina la Serebuka Festival liliandaliwa na Kampuni ya
StarTimes na Kudhaminiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania.
0 Comments