WASOMI WATAKIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO KUKUZA UCHUMI AFRIKA MASHARIKI


  Katibu  mkuu wa Baraza la vyuo vikuu Afrika Mashariki , Profesa Alexandre  Lyambabaje.
 Balozi Ramadahani Mwinyi amabye alimwakilisha waziri wa mambo ya neje na ushirikiano Afrika Mashariki
 baadhi ya washiriki katika kongamano hilo wakifatilia kwa makini.
Mtoa mada wa kwanza  Liliani Awenja akizungumza wakati wa kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam
 Joseph Njogu kutoka  ResearchAfrica akitoa maelezo kwa Balozi Ramadhani Mwinyi alipokuwa akitembelea maonyesho.
 wajumbe kutoka Stramore Univesity ya Nairobi kenya wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni rasmi.
Balozi Ramadhani Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo

Na Humphrey Shao, Dar

WASOMI wanazuoni wametakiwa kutumia maarifa walionayo kwa lengo la kusaidia kukua kwa elimu na Uchumi katika umoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki .

Hayo yamesemwa na Balozi Ramadhani mwinyi, alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga katika ufunguzi wa mkutano wa vyuo vikuu vya Serikali na watu binafsi.

“kama jumuiya lazima tuhakikishe kuwa tunatoa elimu kwa wanataaluma ambayo itawasaidia kuwakwamua kiuchumi kwa kuzalisha wasomi ambao wataweza kutoa ajira kwa wengine na sio wale watakao tegemea ajira kutoka kwa wengine”amesema Mwinyi.

Amesema kuwa elimu inayopatikana kutokana na tafiti mbalimbali zinazofanywa inatakiwa zisadie katika ukuaji wa maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Pages